MMOJA WA WANACHAMA AKIWA AMECHARUKA NA KUPOROMOSHA MANENO KWA RAGE, HII ILIKUWA NI BAADA YA KUZUIWA NA ASKARI. |
Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage,
jana Jumapili alinusurika kuchezea kichapo kutoka kwa wanachama wa klabu hiyo
katika Mkutano Mkuu wa Katiba uliofanyika kwenye Ukumbi wa Maofisa wa Polisi wa
Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Rage alikumbana na balaa hilo baada ya
kuwaita wanachama zaidi ya 1,000 waliohudhuria mkutano huo kuwa ni mbumbumbu na
wenye njaa wakati alipokuwa akihutubia.
ASKARI WAKIENDELEA KUWATULIZA WANACHAMA WA SIMBA WALIOKUWA WANATAKA WAMSHIKISHE ADABU RAGE. |
Maneno hayo ya Rage yaliwaudhi wanachama
hao na baadhi yao wakavamia meza kuu alipokuwa ameketi na viongozi wengine wa
wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo kwa lengo la kutaka kumshushia
kichapo.
RAGE AKIPOROMOSHA 'MIJINENO' KWA WANACHAMA WAKE |
Lakini askari polisi 15 waliokuwa wakiangalia
hali ya usalama ukumbini hapo walifika mara moja na kuzuia tafrani hiyo.
Hata hivyo wanachama hao walimtaka
mwenyekiti wao huyo awaombe radhi ili mkutano huo uweze kuendelea lakini
aligoma jambo ambalo lilizidi kuwafanya wajawe na jazba dhidi yake.
Hata hivyo, baada ya kushauriwa na
baadhi ya wanachama wa klabu hiyo, Rage aliwaomba radhi, wakamsamehe kisha mkutano
huo ukaendelea.
Alifanya hivyo tena mara baada ya
kumalizika kwa mkutano huo ambapo aliwaita wandishi wa habari na kusema:
“Nawaomba wanachama wa Simba wanisamehe kwa lugha yangu ambayo haikuwa nzuri na
sikuwa na lengo la kuwadhalilisha, naomba wanisamehe.”
Katika mkutano huo, Rage ametangaza
kutogombea tena nafasi yake hiyo katika uchaguzi ujao Mei 14, mwaka huu.
Lakini akatupa dongo jingine akidai
aliikuta klabu hiyo ikiwa inanuka kinyesi, chafu na akaahidi kuiacha katika
hali nzuri, tofauti na alivyoikuta.
0 COMMENTS:
Post a Comment