Kocha wa
Simba, Zdravko Logarusic amesema lazima kikosi chake kiongeze wachezaji wazee.
Logarusic
amesema Simba ina wachezaji wengi wenye vipaji lakini inakosa wazoefu.
“Msimu
unakwenda ukingoni, huu ndiyo wakati mwafaka wa kuongeza wachezaji wazoefu kwa
ajili ya kikosi chetu.
“Kama ni
suala la vipaji, wachezaji wetu wengi wana vipaji lakini ninahitaji wenye
uzoefu zaidi. Angalau wachezaji watano wapya,” alisema.
Kuhusiana
na mbio za ubingwa alisema wanaweza kuendelea kupambana lakini akakubali
matumaini yako chini.
0 COMMENTS:
Post a Comment