Kiungo mshambuliaji wa Simba, Ramadhani
Singano ‘Messi’ amevunja vioo vya mlango wa uwanja wa Taifa mara tu baada ya
mechi yao dhidi ya Coasal Union kumalizika.
Katika mechi hiyo, Simba walilala kwa
bao 1-0 na Messi alipoteza nafasi safi katika dakika ya 90 baada ya kubaki yeye
na kipa lakini akashindwa kufunga.
Hali hiyo ilionyesha kumchanganya na
wakati anaingia vyumbani aliupiga teke mlango na kuvunja vioo.
Kutokana na hali hiyo, askari waliingia
na kutaka mumtia nguvuni, lakini Katibu Mkuu wa Simba, Ezekiel Kamwaga
alijitokeza na kuanza kuzungumza nao.
Baada ya mazungumzo hayo ya dakika
kadhaa wakiwa na Kamwaga, askari walionyesha kuiiondoa katika jambo hilo.
Mmoja wa askari hao alisema wameliacha
jambo hilo mikononi mwa Simba na uongozi wa uwanja wa Taifa na kitu kizuri
kwao, aliyevunja mlango huo anajuikana.
0 COMMENTS:
Post a Comment