Mwanariadha nyota wa mbio ndefu wa
Uingereza, Mo Farah ameanguka na kuzimia wakati akimaliza mbio za marathon za New
York City, leo.
Mkali huyo wa Michezo ya Olimpiki
alianguka na kuzimia sekunde baada ya kumaliza na kushika nafasi ya pili nyuma
ya Mkenya Geoffrey Mutai aliyemaliza kwa kutumia dakika 61 na sekunde 8.
Farah, 30, alionyesha kuwa na kasi
katika hatua za mwisho na kufanikiwa kumpita Mkenya mwingine, Stephen Sambu kutoka
nafasi ya tatu hadi aliposhika ya pili.
Aliondolewa na kiti maalum cha wagonjwa
katika eneo hilo na taarifa zilizopatikana baadaye zilieleza alikuwa katika
hali nzuri.
|
0 COMMENTS:
Post a Comment