Baadhi ya kiungo wa Yanga, Frank Domayo
‘Chumvi’ kuonyesha kiwango kizuri na kupiga pasi nyingi za uhakika katika
mchezo wa juzi Jumamosi wa kimataifa dhidi ya Al Ahly, benchi la ufundi la
Waarabu hao limeonekana kumtamani.
Kocha Msaidizi wa Al Ahly ambao ndiyo
mabingwa watetezi wa michuano hiyo ya Ligi ya Mabingwa Afrika, El Sayed
Abdelhariz, amesema Domayo anastahili kuwa miongoni mwa wachezaji wa timu yake.
Abdelhariz alisema Domoyo ndiye mchezaji aliyeharibu mipango yao katika mechi
hiyo iliyokuwa na ushindani mkubwa.
“Tumeyapokea matokea hayo na tunarudi
nyumbani kujipanga kwa ajili ya mechi ya marudiano japokuwa kuna mambo mengi
yaliochangia tukafungwa, kama vile hali ya hewa ambayo ilikuwa ikiwasumbua sana
wachezaji wetu.
“Mipango yetu ilikuwa ni kushinda lakini
mambo yamekuwa tofauti na tulivyotarajia, hata hivyo katika mchezo huo,
mchezaji aliyetusumbua zaidi alikuwa yule aliyekuwa amevaa jezi namba 18
(Domayo), kwani alikuwa anaharibu mipango yetu kila wakati kutokana na uwezo
wake mkubwa wa kukaba na kuanzisha mashambulizi makali kwa kupiga pasi za
uhakika, anastahili kuwa miongoni mwa wachezaji wa kikosi chetu,” alisema Abdelhariz.
0 COMMENTS:
Post a Comment