March 3, 2014


Bekiwa zamani wa Simba, Boniface Pawasa, amesema Simba kwa sasa wasahau suala la ubingwa kabisa na wajipange upya tu ili kuweza kufanya vyema katika msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Simba msimu huu imekuwa haina matokeo ya kuridhisha na imefanikiwa kuvuna pointi mbili tu katika michezo minne iliyopita kabla ya jana.

“Kwa sasa mwenendo wa Simba ulivyo, suala la ubingwa walisahau kabisa na wajipange upya tu ili kuweza kujenga kikosi imara ambacho kitaweza kuwasaidia katika msimu ujao wa ligi kuu na hii huenda imechangiwa na mabadiliko hata ya kocha, kwani (Zdravko) Logarusic ana mfumo wake na anahitaji muda vilevile,” alisema Pawasa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic