Kocha Mkuu wa Azam FC, Joseph Omog, amesema
amekuwa akishindwa kulala vizuri kutokana na kufikiria kuchota pointi 15 katika
michezo yote mitano iliyobaki ili kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Baada ya mchezo wa jana Jumapili dhidi
ya JKT Oljoro kwenye Uwanja wa Chamazi jijini Dar, Azam imebakiza michezo
mitano tu dhidi ya Mgambo, Simba, Ruvu,
Mbeya City na JKT Ruvu.
Omog amesema bado ana kibarua kigumu cha
kuchukua ubingwa wa ligi hiyo kutokana na kuwa na upinzani mkali kutoka kwa
Yanga na Mbeya City.
Omog
amesema ni vigumu kujihakikishia nafasi ya ubingwa katika kipindi hiki kwa kuwa
kuna mechi nyingi ngumu ambazo itabidi akabiliane nazo.
“Mechi sita zilizobakia ni nyingi sana,
hivyo siwezi kusema kama nitachukua ubingwa wa ligi kwa kuwa, kila timu
inajipanga ili ishinde, tutajipanga kufanya vizuri katika michezo inayofuata
ili tujiweke katika mazingira mazuri.
“Matokeo ya leo ni mazuri na wachezaji
wameonyesha kiwango, tunahitaji kuimarika zaidi ili tufanye vizuri,” alisema
Omog.
0 COMMENTS:
Post a Comment