Shabiki wa Yanga aliyefahamika kwa jina
la Joseph William, mkazi wa Gongo la Mboto, Dar es Saalam, alipasuliwa paji la
uso na mashabiki wenzake uwanjani, hali iliyosababisha ashonwe nyuzi zaidi ya
12 huku mwenzake mmoja, Hamza Abdallah wa Ilala, akichanwa pembeni ya uso baada
ya kupigwa na nati za kufungia viti.
Matukio hayo yalitokea juzi katika
mchezo wa Yanga dhidi ya Al Alhy uliochezwa
Uwanja wa Taifa jijini Dar na Yanga kuibuka na ushindi wa 1-0.
Mashabiki hao walipata majeraha baada ya
kuwa wanagombana uwanjani kwa kutupiana viti wakati mechi ikiendelea lakini
hali zao zinaendelea vizuri.
Mashabiki hao wa Yanga walikuwa wakitupiana
viti na mashabiki wanaodaiwa ni wa Simba waliokuwa wanaisapoti Al Ahly.
Akizungumza na Championi Jumatatu, mmoja
madaktari wa huduma ya kwanza uwanjani hapo, aliyefahamika kwa jina moja la
Nassor, alisema majeruhi hao walipata matibabu
hapo.
“Mashabiki hawa wawili ndiyo tuliowapokea
na wote ni wa Yanga, wamepata majeraha baada ya kutupiwa viti pale uwanjani wakati
mchezo ukiendelea, Joseph William wa Gongo la Mboto kashonwa nyuzi zaidi ya
12,” alisema daktari huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment