Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, ameitabiria
makubwa timu ya Yanga kuwa itawafunga tena Al Ahly ya Misri kwenye mechi yao ya
marudiano.
Yanga juzi ilishinda kwa bao 1-0 huku ikitarajia kurudiana na
wababe hao baada ya wiki moja huko Cairo, Misri.
Sadick alikuwa mmoja wa viongozi waliohudhuria mtanange huo ambapo
alisema amefurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wa Yanga ambacho
kinampa moyo kuwa Yanga itafanya vizuri kwenye mchezo wa marudiano.
Alisema kuwa ameiona Ahly kuwa haina nguvu, wazito na mwisho
kabisa si wajanja wa kuweza kuifunga kwa wepesi hata kama wakiwa kwao, hivyo
hana tatizo juu ya Yanga kwenye mechi yao hiyo inayotarajiwa kuwa ngumu.
“Wale hawatuwezi, tuliwazidi kila sehemu, mpira wote tumecheza
sisi, hawana stamina, halafu si wajanja wa kuweza kuwazidi wachezaji wa Yanga,
tutawafunga tena huko kwao wala tusiwe na wasiwasi,” alisema Sadick.
0 COMMENTS:
Post a Comment