Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) lilifikia makubaliano na kampuni ya Adidas kupitia msaada wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kupatiwa vifaa vya michezo.
Awali Stars ilikuwa inatumia jezi aina ya Uhlsports ambazo ni kati ya vifaa bora vya michezo.
Hata hivyo, TFF haijaweka wazi kuwa kwa nini imeachana na Uhlsports na itafaidika vipi katika kutumia jezi hizo za Adidas ambayo ni kampuni kubwa zaidi ya vifaa vya michezo duniani.
Kufuatia makubaliano hayo TFF
tulipatiwa vifaa kadhaa vya adiads kwa ajili ya timu ya Taifa ya wakubwa (Taifa
Stars). Vifaa hivyo zikiwemo jezi tulianza kuvitumia kwenye mechi ya kirafiki
dhidi ya Namibia iliyochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek.
Vifaa hivyo zikiwemo jezi vitaendelea
kutumiwa na Taifa Stars hadi hapo utaratibu mpya wa jezi za timu ya Taifa
utakapokamilika.
TFF tunaishukuru kampuni ya Adidas
ambao ni washirika wa CAF na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)
kwa miaka mingi kwa mchango wao huu wa kuendeleza mpira wa miguu nchini.
0 COMMENTS:
Post a Comment