April 11, 2014

 
SHEARER
Na Saleh Ally
MWENDO wa upachikaji mabao kwenye Ligi Kuu England kwa sasa, gumzo ni ule wa mshambuliaji wa Liverpool, Luis Suarez ambaye amefikisha 29.

Suarez yuko kileleni na mabao hayo akifuatiwa na na patna wake, Daniel Sturridge mwenye 10, halafu Yaya Toure wa Man City mwenye 17. Inaonekana hakutakuwa na mwenye uwezo wa kumkamata raia huyo wa Uruguay ingawa kwenye soka mambo yanaweza kubadilika wakati wowote.

Lakini kama utazungumzia wafungaji wanaoendelea kucheza katika ligi hiyo hadi sasa, Wayne Rooney na Robin van Persie wa Manchester United ndiyo wamefunga mabao mengi zaidi.

Rooney na van Persie wanajitutumua kwa kuwa ndiyo washambuliaji pekee wanaoendelea kupambana kwenye ligi hiyo wako kwenye kumi bora ya waliofunga mabao mengi England.
Lakini kama utataka kuangalia mshambuliaji yupi ni mkali zaidi, basi Alan Shearer aliyewahi kukipiga Blackburn Rovers na Newcastle ndiye kiboko yaw engine wote unaowajua.
ROONEY

Shearer ambaye alichipukia kisoka katika Southampton hakucheza soka katika moja ya timu ambazo zinaonekana ni kubwa kama vile Arsenal au Manchester United.
Lakini anaendelea kuongoza kwa kushikilia rekodi ya mfungaji bora zaidi wa Premiership baada ya kufunga mabao 260 katika mechi ya 441, hii ni tokea msimu wa 1992 hadi 2006.
Shearer anaaminika mmoja wa wachezaji wenye uwezo mkubwa zaidi wa kufunga na si England tu, badala yake hata anapolinganishwa na washambuliaji wengine nyota duniani.
Wakati fulani baada ya Robbie Fowler alipoanza kutamba Liverpool na kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England, baadhi ya wachambuzi walitaka apewe nafasi na Shearer kuwekwa kando.
Lakini Fowler aliwashangaza wengi baada ya kuwajibu wachambuzi kwamba hawakuwa wakimjua vizuri Shearer ambaye alikuwa akifunga asilimioa 90 ya mipira aliyopiga wakiwa mazoezini na Fowler alifunga asilimia 68 hadi 75 tu.
Hivyo akawataka kuendelea kumuamini mkongwe huyo ambaye kweli aliendelea kutamba kwa miaka mingine minne.
Rooney na van Persie wana nafasi ya kumfikia Shearer lakini si kwa asilimia nyingi kwa kuwa nafasi wanazoshika katika 10 bora hiyo si za juu sana.
Rooney anajikongoja zaidi akiwa katika nafasi ya nne, ana mabao 171 baada ya kucheza mechi 367, wakati van Persie anashika nafasi ya 10 kwa mabao yake 132 katika mechi 247.
Bado inaonyesha hivi, kwa mwendo wao itakuwa kazi kubwa kumfikia mkongwe huyo aliyestaafu zaidi ya miaka saba iliyopita.
Katika wachezaji 10 ambao wako kwenye listi ya waliofunga mabao mengi zaidi wawili tu ndiyo wanaoendelea kucheza na wengine nane walishastaafu akiwemo Shearer mwenyewe.
Kama Rooney au van Persie watashindwa kumfikia Shearer, maana yake kwa kipindi cha miaka watakayokuwa wakicheza, huenda ikachukua miaka mingine 20 mmoja wapo kutokea na kumpita mkali huyo.



Msimu
Mabao
Mechi
1992–2006
260
441
1992–2008
188
414
1999–2007, 2012
175
258
2002–
171
367
1995–
170
573
1993–2009
162
378
1996–2013
150
325
1992–2005
149
351
1992–2007
147
418
2004–
132
247


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic