Mshambuliaji Kun Aguero amerejea na
kuanza kwa kasi baada ya kuisaidia Man City kuitwanga Wes Brom mabao 3-1.
Aguero aliyekuwa majeruhi, alifunga bao
la pili katika dakika ya 10 baada ya Pablo Zabaleta kuanza mapema kuipatia City
bao la kuongoza katika dakika ya 3 tu.
Dorrans aliifungia Wes Brom iliyokuwa
ugenini bao na kufanya mechi iwe na ushindani mkubwa zaidi lakini Demichelis
akafunga bao la tatu katika dakika ya 36 na kuwavunja nguvu wageni wao.
Kutokana na ushindi huo, City imefikisha
pointi 74 nyuma ya Chelsea wenye 75 na vinara wa ligi hiyo Liverpool, wenye 80.
Hata hivyo, City wana mchezo mmoja mkononi.
0 COMMENTS:
Post a Comment