Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic
amesema ndani ya siku chache atarejea kwao Croatia.
Loga amesema ameamua kuondoka kabla ya
kupata mkataba mpya wa Simba kwa kuwa mambo yanakwenda taratibu.
“Mambo yanakwenda taratibu sana na muda
unakimbia, acha nirudi nyumbani kwanza.
“Nafikiri ndani ya siku tatu nitakuwa
nimerejea nyumbani. Hivyo mengine tutajua,” alisema.
Klabu ya Simba imesema ina siku kadhaa
ya kujadili suala lake na ikaomba subira itangulizwe.
Lakini kocha huyo amesisitiza, ukifika
wakati wa kuondoka, hatajali kama tayari kapewa mkataba mpya au la.
0 COMMENTS:
Post a Comment