OLJORO |
Rhino ya Tabora, Ashanti United
na JKT Oljoro rasmi wameteremka daraja na kurejea Ligi Daraja la Kwanza.
Ashanti imeshuka baada ya kuchapwa bao
1-0 na Prisons ya Mbeya katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini
Morogoro, leo.
ASHANTI UNITED |
Wachezaji wa Ashanti United, walilia kwa
uchungu wakionyesha kutofurahia kuteremka daraja.
Rhino nao wakiwa nyumbani Tabora, leo
wamepigwa mabao 2-0 na Ruvu Shooting. Hamis Mohammed na Elias Maguri ndiyo
walioimaliza timu hiyo ya Tabora.
RHINO |
Mjini Arusha, JKT OLjoro wameteremka
rasmi baada ya kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar. Timu hiyo ya jeshi
inakuwa timu ya tatu kuteremka daraja.
Kutokana na kuteremka kwa timu hizo,
Ndanda FC, Stand ya Shinyanga na Polisi ya Morogoro ndiyo wamepanda rasmi Ligi
Kuu Bara.
0 COMMENTS:
Post a Comment