Bondia nyota wa Tanzania, Francis Cheka
ameshindwa kuonyesha makali yake baada ya sare dhidi ya Gavad Zohrehvand wa
Iran.
Katika pambano hilo lisilo la kuwania
ubingwa, lililopigwa usiku wa kuamkia leo. Zohrehvand alionekana kuwa fiti
kuliko wengi walivyotarajia.
Mgeni huyo alimpa wakati mgumu Cheka, hali
iliyosababisha baadhi ya mashabiki waliokuwa kwenye Ukumbi wa PTA, Temeke
jijini Dar, walipinga waziwazi matokeo hayo.
Baada ya pambano hilo, Zohrehvand
naye alisisitiza kwamba alishinda licha ya majaji kumbeba Cheka waziwazi.
0 COMMENTS:
Post a Comment