Mabingwa wapya wa Tanzania, Azam FC,
wamekabidhiwa rasmi kombe lao na Rais wa TFF, Jamal Malinzi.
Kombe hilo limekabidhiwa baada ya Azam
FC kukipiga na JKT Ruvu na kuichapa timu hiyo ya jeshi kwa mabao 1-0 ambayo
imeteremka daraja.
Bryan Umonyi, raia wa Uganda ndiye
alifunga bao hilo baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Kipre Tchetche.
Hadi wanakabidhiwa kombe, mechi hiyo
ilikuwa imejaza watu wengi na mashabiki wakiwa wengi kwa kuwa pambano hilo
halikuwa na kiingilio.
Lakini pia kulikuwa na shoo kutoka kwa
vikundi mbalimbali wakiwemo Wanaume TMK walioongozwa na Mheshimiwa Temba.
0 COMMENTS:
Post a Comment