April 19, 2014


Kipa wa Simba, Ivo Mapunda amelalama kitendo cha mshambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu kukimbia na taulo lake.

Kavumbagu alilitoa langoni taulo la Ivo na kwenda kulirusha kwa mashabiki, lakini baadaye Simba walimpelekea taulo lingine.

Dakika chache baada ya taulo mpya, shabiki wa Yanga aliruka uzio na kwenda kulichukua na kulirusha kwa mashabiki huku askari wakiangalia na wakiwa kimya.
Matukio yote hayo yametokea leo katika mechi ya kufunga dimba la Ligi Kuu Bara iliyowakutanisha watani, Yanga na Simba kwenye Uwanja wa Taifa na game ikaisha kwa kumaliza ubishi wa sare ya bao 1-1.
Hali hiyo imemfanya Ivo alaumu kuhusiana na kitendo hicho huku akisema hakikuwa cha kiungwana hata kidogo.
“Taulo ndiyo nilikuwa ninatumia kujifuta au kufuta glavu zangu, mwamuzi mwenyewe aliruhusu liwe pale. Sasa wao wanapolitupa maana yake hata mwamuzi hakuwa sahihi.
“Lakini kwa hali ya kimichezo si sahihi kwa kuwa hatuendi pale kwa ajili ya uadui, si kitu kizuri na si kitendo cha kimichezo,” alisema Mapunda.
Nchini Kenya, Taulo la Mapunda, limekuwa maarufu sana kwa mashabiki wa Gor Mahia ambao wanaamini likiwa langoni, kipa huyo hudaka mikwaju mingi ikiwemo ya penalty.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic