Mashabiki wamezidi kuonyesha kuzidiwa na
mapenzi kila inapochezwa mechi ya watani Yanga na Simba.
Baadhi ya mashabiki wamezimia leo baada
ya Simba kupata bao katika dakika ya 82, wakabebwa na kupatiwa huduma ya kwanza.
Dakika chache baadaye Simon Msuva
akaisawazishia Yanga, ilikuwa katika dakika ya 85.
Baada ya hapo, mashabiki wengine wa
Yanga walioshituka kwa furaha na wale wa Simba, waliotishwa na bao hilo,
wakazimia pia.
Watu wa msalaba mwekundu wakaanza kufanya
kazi ya ziada kuhakikisha wanawapa huduma.
Timu hizo zilimaliza mechi hiyo kwa sare
ya mabao 1-1 na kumaliza ubishi kuwa nani ni zaidi ya mwenzake.
0 COMMENTS:
Post a Comment