Kipa namba moja wa Simba, Ivo Mapunda,
amesema wamejipanga vyema kuhakikisha wanaifunga Yanga katika mchezo wa leo.
Yanga na Simba zinatarajiwa kukutana leo
Jumamosi katika Dimba la Taifa jijini Dar es Salaam kwenye mchezo wa hitimisho
la msimu wa ligi kuu 2013/2014.
Mchezo huo wa watani wa jadi unatarajiwa
kuwa na ushindani mkubwa ikiwa kila upande ukihitaji kujenga heshima.
Ivo ambaye ni kipa wa zamani wa Yanga, alisema wanahitaji kufanya maandalizi ya kufa mtu ili waweze kushinda mchezo
huo.
“Kushinda na kushindwa ni matokeo ya
mpira kwani mpira ni dakika 90, lolote linaweza kutokea lakini sisi tumejipanga
kuhakikisha tunamfunga mpinzani wetu kwa lengo la kulinda heshima yetu.
0 COMMENTS:
Post a Comment