Na Saleh
Ally
KUANZIA
leo, kesho na keshokutwa utakuwa ni mtihani mkubwa kwa timu zinazowania ubingwa
kwa kuwa zinakutana na timu ambazo lazima zishinde au hazina cha kupoteza.
Timu
zinazopambana kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England ni Liverpool, Manchester City
na Chelsea huku ikionekana Arsenal wamebaki kwenye zile mbio zao za kila msimu,
kuwania kupata nafasi katika nne bora ili washiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Lakini hao
wanaopambana kupata ubingwa, wiki hii wana mechi ambazo mwendo wake unaonyesha
lazima kunaweza kutokea kwa hali ya kushangaza hasa kama hawatakuwa makini.
Takwimu za
Ligi Kuu England maarufu kama Premiership inaonyesha hivi, timu zinazokuwa
kwenye hatari ya kuporomoka daraja, zimekuwa ni msumari kwa kuwa zimekuwa zikizikosesha
ubingwa timu zilizo juu kwa asilimia 69.
STOKE KAZINI KUIZUIA CHELSEA.. |
Wakati zile
timu ambazo ziko katika hali ya kutokosa lolote, kwamba hazitateremka daraja au
kuchukua ubingwa, nazo zimezikosesha zile zilizokuwa zinawania ubingwa nafasi
hiyo kwa asilimia 54.
Hivyo timu
ambazo zinawania kuepuka kuteremka daraja ndizo hatari sana kwa timu zinazotaka
kuwa bingwa na ratiba ya leo, kesho Jumapili na keshokutwa Jumatatu zinaonyesha
Chelsea, Man City, Liverpool na Arsenal zitakuwa na wabishi hao.
Timu
zinazokaribia kuteremka daraja ambazo zinapambana kuepuka kuanguka, kawaida
zimekuwa zikiongeza kiwango kwa zaidi ya asilimia mia katika mechi zao nane za
mwisho za msimu.
Hivyo
kukutana na timu ambayo inakaribia kuteremka daraja, wakati unapambana kupata
ubingwa, mechi inakuwa na presha mara mbili zaidi ya kawaida.
JUMAMOSI:
Chelsea Vs
Sunderland
Katika
mechi nane za mwisho, Chelsea bado ina rekodi nzuri kwa kuwa imeshinda sita na
kupoteza mbili tu. Hivyo ni ya kiwango cha juu kama utailinganisha na
Sunderland ambayo inashikilia mkia, imetoka sare mbili na kupoteza sita
zilizobaki.
Lakini hapo
ndiyo utajua maana ya mchezo wa soka kuwa na mashabiki wengi zaidi kwa kuwa hautabiriki
hata kidogo, kwani Sunderland tayari imeitoa Man City ‘jasho la meno’ baada ya
vijana hao wa Manuel Pellegrini kujikuta wanapambana kusawazisha.
Sunderland
wana pointi 26 wakiwa wamebeba timu zote 19, lakini bado wanaamini wanaweza
kuokoka na wanataka kushinda. Chelsea wana 75 katika nafasi ya pili, wanajua
wakiteleza mechi moja, wataiachia njia Man City kwenda kupambana na Liverpool.
Vijana hao
wa Jose Mourinho wanataka kuendelea kutopoteza nyumbani, hivyo ni vita
isiyokuwa na mwenyewe.
JUMAPILI:
Hull City
Vs Arsenal:
Unaweza
kusema ni mechi ya majaribio ya fainali ya Kombe la FA. Maana hizi ndiyo timu
zitakazocheza siku hiyo, lakini safari hii ni mawazo tofauti kabisa kwa kuwa
Arsenal wanataka nafasi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na Hull City, hawana cha
kupoteza lakini wanatakiwa kushinda na kujiweka vizuri kwa kuwa pointi 36,
haziwahakikishii kwa asilimia kubaki.
Itakuwa
mechi ngumu kwa kuwa Hull City waliopoteza mechi mbili kabla, waliibuka na
kushinda, hivyo ni lazima wajihakikishie nafasi ya kubaki.
Norwich Vs
Liverpool:
Norwich
wana pointi 32, wakichezea nafasi wameumia na Liverpool wanajua wakikosea, basi
Chelsea na Man City watawadhuru, hivyo hakuna utani.
Norwich
wamepoteza mechi zao zote tatu za mwisho, lakini wanajua matumaini yao yanaweza
kupatikana kupitia vijana hao wa Anfield ambao watakuwa wageni wao kesho.
JUMATATU:
Man City Vs
Wes Brom
Man City
wana hofu kwa kuwa mechi yao ya mwisho wamelazimisha sare ya mabao 2-2 dhidi ya
Sunderland wakiwa wametoka kupigwa mabao 3-2 dhidi ya Liverpool.
Wes Brom
wanajulikana kwa ubishi, hakutakuwa na utani kwa kuwa mechi yao ya mwisho
walitoka sare na wenyewe wanataka kubaki ligi kuu kwa kuwa wana pointi 33.
Maana yake
itakuwa ni vita ya anayetaka kubaki na aliyepania kuchukua kombe, si kazi
Rahisi. Hata hivyo Wes Brom hawana rekodi nzuri ya ugenini kwa kuwa katika
mechi 16, wameshinda tatu tu.
0 COMMENTS:
Post a Comment