KAVUMBAGU (MWENYE KOFIA KATIKATI) AKIWA KATIKA KIKOSI CHA YANGA KILIPOWASILI JIJINI CAIRO |
Mshambuliaji Didier Kavumbagu wa Yanga, kwa mara ya kwanza amefunguka kuhusiana na timu hiyo kukosa ubingwa katika hatua za mwisho.
Kavumbagu ameiambia
SALEHJEMBE kuwa, kushindwa kuitoa Al Ahly kulishusha ari ya wachezaji wa Yanga
na kusababisha wengi kucheza chini ya kiwango.
Mshambuliaji huyo mrefu
na mwenye purukushani nyingi amesema Yanga ilianza kupotea baada ya kurejea
kutoka Misri.
“Tuliona kuwa
tulistahili kabisa kuitoa Al Ahly, baada ya kushindwa ilimuumiza sana kila mtu.
Hivyo tuliporejea kwenye ligi, mambo hayakuwa mazuri.
“Utaona tulishindwa
kufanya vizuri, tukaanza kutoka sare mechi tulizotakiwa kushinda.
WACHEZAJI WA YANGA WAKIWA KWENYE BENCHI BAADA YA KUPOTEZA MECHI DHIDI AL AHLY JIJINI ALEXANDRIA. |
“Lakini mambo yakawa
mabaya zaidi kwa sababu tulifikia hadi kupoteza kwa Mgambo kule Tanga. Hapo ndiyo
tulipotea na kuwapa Azam nafasi ya kutwaa ubingwa.
“Lakini hauwezi kusema
Yanga ilikuwa na kikosi kibaya, ina kikosi kizuri na kinaweza kushinda dhidi ya
timu yoyote ile,” alisema.
Katika mechi mbili za
Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri, Yanga ilianza kwa kuifunga
timu hiyo bao 1-0 jijini Dar ingawa ilistahili kushinda.
Ikapoteza kwa idadi
hiyo ya bao 1-0 mjini Alexandria, mechi ikaenda katika mikwaju ya penalti bado
Yanga ikapoteza licha ya kwamba ilikuwa na nafasi zaidi ya wenyeji kusonga mbele.
0 COMMENTS:
Post a Comment