April 26, 2014

TAMBWE AKIPAMBANA

Mshambuliaji nyota wa Simba, Amissi Tambwe amesema yuko tayari kucheza timu yoyote iwe Yanga au mabingwa Azam FC.

Tambwe raia wa Burundi amesema hadi sasa ana mkataba wa mwaka mmoja na Simba, lakini anachosubiri ni ofa.
“Kama Simba watakuwa wnaanihitaji, sawa hakuna tatizo kwa kuwa ndiyo timu yangu.
“Lakini kama hawanitaki, pia niko tayari kwenda na kuichezea timu yoyote. Iwe Azam, Yanga au nyingine.
“Sasa ninaipenda sana Simba, lakini nikihamia timu nyingine nitaipenda pia kwa kuwa ndiyo kazi yangu,” alisema Tambwe.

Tambwe ndiye mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara na ndiye amekuwa mshambuliaji kivutio zaidi kwa msimu uliomalizika Simba ikishika nafasi ya 4.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic