April 26, 2014


Kila mechi itakayochezwa leo itatoa heshima ya mwisho kwa kocha wa zamani wa Barcelona, Tito Vilanova kwa wachezaji na mashabiki wote kusimama kimya kwa dakika moja.

Shirikisho la Soka la Hispania limeagiza timu zote kusimama na kufanya hivyo, leo, kesho na keshokutwa.
Mechi ya kwanza ambayo itashiriki katika kutoa heshima kwa Vilanova aliyefariki jana akiwa na umri wa miaka 45 ni ile itakayozikutanisha Elche dhidi ya Levante.

Lakini hata shirikisho la mpira wa kikapu nchini humo limeagiza mechi zote za wikiendi kuwe na kipande hicho cha dakika moja kutoa heshima kwa Vilanova na mechi ya kwanza kufanya hivyo itakuwa ile kati ya ya Real Madrid dhidi ya Olympiacos ambayo ni ya michuano ya kikapu barani Ulaya.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic