Beki wa kati wa Simba na timu ya taifa
ya Burundi, Gilbert Kaze, ameweka bayana kuwa, anawasubiri Simba wampe chake
aende kwao akapumzike.
Licha ya uongozi wa Simba kutotaka
kuweka wazi hatma ya beki huyo msimu ujao, lakini taarifa chini ya kapeti
zinasema nyota huyo ameonyeshwa mlango wa kutokea kwa kile kilichodaiwa ni
kiwango kidogo pamoja na kuwa nje kwa muda mrefu akisumbuliwa na jeraha la
goti.
Kaze alikiri kusikia taarifa hizo na
kusema kuwa anawasubiri Simba wamkatie chake ili atimke na kuongeza kuwa hawezi
kucheza tena Tanzania baada ya kutemwa Simba.
“Nasikia taarifa kama hizo na kama zina ukweli,
sawa, mimi nasubiri Simba wanipe fedha zangu, maana nina mkataba wa mwaka na
nusu mbeleni, nilisaini miaka miwili na nusu. Kwa hiyo kama wameamua kuniweka
pembeni poa tu.
“Lakini ukweli ni kwamba siwezi kubaki
Tanzania iwapo nitaondoka Simba, nitakwenda nyumbani ili nijitibu goti kisha
nitaangalia timu hukohuko, ila siyo hapa Tanzania,” alisema beki huyo aliyeiokoa
Simba kutofungwa na Yanga msimu huu, kwa bao lake la dakika 84 lililoipa sare
ya mabao 3-3.
0 COMMENTS:
Post a Comment