April 28, 2014





Kipa wa Yanga, Juma Kaseja, juzi Jumamosi alijikuta akiwa katika wakati mgumu baada ya kuvamiwa na mashabiki wa Simba, waliozingira gari lake wakimtaka arudi Msimbazi.


Nahodha huyo wa zamani wa Stars, alijikuta akiwekwa ‘mtu kati’ wakati akitoka Uwanja wa Taifa kushuhudia timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars), ikiadhibiwa mabao 3-0 na Burundi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.

Katika tukio hilo lilishuhudia tukio hilo ambapo mashabiki hao waliorundikana katika geti kuu la Uwanja wa Taifa, walizingira gari la Kaseja huku wakimuita kwa huzuni na wengine wakimwambia: “Kaseja..Kaseja.. rudi Simba basi, urudi nyumbani kwenu na siyo huko Yanga wanaokunyanyasa.”

Katika tukio hilo, Kaseja hakutaka kujibu lolote ambapo aliondoka huku akicheka.
Nyota huyo alitua Jangwani wakati wa dirisha dogo msimu uliomalizika akitokea mitaani, kufuatia kutemwa na Simba baada ya kumaliza mkataba, akiwa ameshaitumikia kwa miaka 10.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic