April 28, 2014





Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers amesema Chelsea walipaki mabasi mawili wakati wa mechio dhidi yao ambayo wageni hao kutoka London walishinda kwa mabao 2-0 na kuwatibulia mbio za ubingwa.



Akizungumza baada ya mchezo huo wa Ligi Kuu England, Rodgers alisema basi la kwanza walilopaki Chelsea ni namna walivyoweka mabeki wengi nyuma na kucheza kwa kujilinda zaidi.

Pili ni kocha wao Jose Mourinho ambaye alikuwa akifanya makusudi kuchelewesha mpira.

Alisema Mourinho alichelewesha mpira kwa makusudi na kumtafsiri kama basi la pili.
Pamoja na kushambulia sana, Liverpool hawakupata bao huku Chelsea wakifunga mabao yao mawili kila mwisho wa kipindi. La kwanza dakika ya 45 na la pili dakika ya 90.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic