Kocha Mkuu wa
Simba, Zdravko Logarusic, amesema ili kikosi cha Simba kiwe bora msimu ujao, ni
vyema wakasajiliwa wachezaji wenye viwango vya hali ya juu ili kurudisha
heshima ya timu.
Simba
imemaliza ligi ikiwa katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 38, nyuma ya Mbeya
City yenye pointi 46.
Loga amesema
lazima ufanyike usajili mkubwa msimu ujao ili kuwa na kikosi bora katika nafasi
zote kwa kusajili wachezaji wenye hadhi ya kuichezea Simba ambao wataleta
ushindani.
“Simba
inahitaji marekebisho makubwa katika nafasi zote kuanzia kipa hadi
washambuliaji, wachezaji wanaotakiwa kusajiliwa wawe na hadhi pamoja na viwango
vya kuweza kuichezea Simba na si kama ilivyo sasa wachezaji wengi siyo wazuri.
“Sijajua
mchezaji gani anafaa lakini wanatakiwa kusajili sehemu yoyote watakapoona kuna
mchezaji anayefaa ili kuwa na kikosi bora.
“Bado uongozi
unatafuta wachezaji kutoka sehemu mbalimbali,” alisema Loga.
0 COMMENTS:
Post a Comment