Mwenyekiwa Klabu ya Azam FC, Said
Mohammed, amerusha kombora kwa wanachama na mashabiki wa Yanga ambao wamezidi
kuiandama Azam kuwa imenunua ubingwa.
Katika mechi za mwishoni kabla ya
kumalizika kwa ligi, Azam imekuwa ikishutumiwa kutumia njia za mkato kwa kile
kilichodaiwa na mashabiki wanaosadikika kuwa wa Yanga kwamba wanatoa hongo ili
watwae ubingwa.
Said
amesema anawafananisha Yanga na kioo kwa mantiki
kwamba kama kweli Azam walihujumu basi nao ubingwa wowote ambao wamekuwa
wakitwaa walikuwa wakihujumu.
“Tuhuma hizo nazifananisha na kioo. Kioo
ukikitazama lazima ujiangalie mwenyewe. Kwa hiyo linalosemwa kama kweli wana
uhakika kuwa tumekuwa tukihonga timu ili ziachie pointi, basi na sisi tuamini
ndiyo imekuwa njia yao ya ubingwa,” alisema bosi huyo.
Azam walitwaa ubingwa wa msimu wa
2013/14 kwa rekodi ya kutopoteza mchezo wowote kama walivyofanya Simba mwaka
2009.
0 COMMENTS:
Post a Comment