Real Madrid imeivua rasmi ubingwa Bayern Munich na kufanikiwa kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ndani ya miaka 12.
Madrid imeshinda mabao 4-0 katika mechi
yake ya pili ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa iliyochezwa kwenye Uwanja wa
Allianz Arena jijini Munich, leo hivi punde.
Maana yake, Madrid imetinga fainali kwa
jumla ya mabao 5-0 baada ya ushindi wa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Santiago
Bernabeu jijini Madrid.
Bayern Munich inayofundishwa na Pep Guardiola, kocha wa zamani wa Barcelona aliyekuwa akiisumbua sana Madrid, leo ilitarajiwa kuonyesha uwezo mkubwa na kuishangaza Madrid iliyotangulia kushinda 1-0 nchini Hispania, lakini haikuwa hivyo.
Mabao ya mchezo ulioisha hivi punde,
yalifungwa na Sergio Ramos na Cristiano Ronaldo kila mmoja akifunga mawili.
Madrid ilionyesha soka la kuvutia na
walikuwa hatari kwa mashambulizi ya kushitukiza yaliyowapa shida wapinzani wao.
Ramos alifunga mabao yake yote katika
kipindi cha kwanza kilichomalizika kwa Madrid kuwa mbele kwa mabao 2-0.
Ronaldo akamaliza kazi kipindi cha pili
akianza kupata pasi safi ya Gareth Bale aliyegongeana na Karim Banzema kabla ya
kufunga la pili kwake na la nne kwa Madrid ikiwa imebaki dakika moja mpira
kwisha.
0 COMMENTS:
Post a Comment