April 30, 2014


Na Saleh Ally
USHINDI wa jana wa mabao 3-0 dhidi ya Newcastle umeiweka Arsenal katika mazingira mazuri ya kujihakikishia kushika nafasi ya nne na kupata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Arsenal imefikisha pointi 73 huku ikiwa imebakiza mechi mbili mkononi lakini itatakiwa kushinda moja kati ya hizo mbili ilikuwa na uhakika kabisa kwa kuwa Everton inaweza kuwa kimeo kwao.
Everton ina pointi 69 mkononi ikiwa na mechi mbili kama za Arsenal ambayo kama itapoteza mechi zake mbili zilizobaki na Everton ikashinda zote itakuwa imeharibu mipango.
Arsenal inayoongozwa na Arsene Wenger tokea mwaka 1986 ni moja ya timu kubwa England na maarufu duniani kote, lakini ina tatizo kubwa.
Tatizo la Arsenal imekuwa ni timu inayowania kupata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya hata kuliko ubingwa, kitu ambacho kinawachanganya mashabiki wengi wa kikosi hicho.
Hakuna timu inayocheza soka la kuvutia kama Arsenal kwa England. Wanajua kupangilia mambo na pasi za uhakika, hata mabao yao mengi yamekuwa ya kuvutia kwa kuwa kandanda lao haliendani na lile la Kiingereza kwa asilimia kubwa.
Wanacheza kwa mipango, uhakika wa mambo na wakikupatia basi wanakufunga mabao mengi. Lakini tatizo inaonekana kama hawana habari na ubingwa na nafasi nne za juu zinawatosha sana.
Katika msimu mitatu iliyopita ukijumlisha na huu wa 2013-14, utaona Arsenal imeishia katika moja ya timu nne zilizoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Lakini bado ni ajabu, katika misimu minne inaonyesha Arsenal imeshika nafasi ya nne mara tatu na nafasi ya tatu mara moja tu.
Rekodi zinaonyesha katika misimu yote, Arsenal ndiyo timu iliyoongoza ligi kwa asilimia kubwa ikichuana na Manchester United ya Alex Ferguson lakini mwisho inaishia nafasi ya nne!
Msimu wa 2010-11, Arsenal iliishia katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 68, wapinzani wao wakubwa Man United wakawa mabingwa baada ya kujikusanyia pointi 80 ikiwa ni tofauti ya pointi 12 na bingwa.
Halafu msimu wa 2011-12 ikajitutumua na kumaliza katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 70 na Manchester City wakawa mabingwa wakiwa na pointi 89, ikiwa ni tofauti ya pointi 19 na mabingwa.
Msimu wa 2012-13
Wakarudi kwenye nafasi yao ya nne wakiwa na pointi 73 na bingwa akawa Manchester United akiwa na pointi 89, ikiwa ni tofauti ya pointi 16.
Safari hii msimu huu, tayari vinara Liverpool wenye pointi 80 na wana uwezo wa kufikisha pointi 86 wakishinda mechi zao mbili zilizobaki na Man City wenye mechi tatu pia wanaweza kufikisha pointi hizo.
Arsenal wakishinda zote zilizobaki, wana nafasi ya kufikisha pointi 79 na kama Chelsea mwenye pointi 78 akishinda mechi moja katika mbili alizonazo maana yake Arsenal itakuwa imejihakikishia nafasi ya nne na si zaidi ya hapo.
Angalia rekodi ya misimu yote minne, Arsenal imekuwa ikishindwa kuvuka pointi 70 na kuingia kwenye 80 na huenda ndiyo tatizo lao linalowabakiza katika nne bora au nafasi ya nne na kupata nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Arsenal ni timu isiyokuwa na mwendo wa uhakika, kwamba inapokaa kileleni, basi inakuwa vigumu kuishusha. Inaonyesha ina ‘pumzi’ mwanzoni mwa msimu lakini kila unapozidi kwenda ukingoni, basi taratibu inaporomoka na mara nyingi inakwama namba nne. Kweli Arsenal ni wazee wa 4!
 2013-14
#
Team
GP
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
36
25
5
6
96
46
50
80
2
36
24
6
6
69
26
43
78
3
35
24
5
6
93
35
58
77
4
36
22
7
7
65
41
24
73

2012-13
Pos
Team
Pld
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
Qualification or relegation
1
38
28
5
5
86
43
+43
89
2
38
23
9
6
66
34
+32
78
3
38
22
9
7
75
39
+36
75
4
38
21
10
7
72
37
+35
73



2011-12
os
Team
Pld
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
Qualification or relegation
1
38
28
5
5
93
29
+64
89
2
38
28
5
5
89
33
+56
89
3
38
21
7
10
74
49
+25
70
4
38
20
9
9
66
41
+25
69


2010-11
Os
Team
Pld
W
D
L
GF
GA
GD
Pts
Qualification or relegation
1
38
23
11
4
78
37
+41
80
2
38
21
8
9
69
33
+36
71
3
38
21
8
9
60
33
+27
71
4
38
19
11
8
72
43
+29
68







0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic