Na
Saleh Ally
MECHI
mbili za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kati ya mabingwa watetezi
Bayern Munich dhidi ya mabingwa wa England, Manchester United, zilitarajiwa
kuzaa mambo mengi sana.
Kazi
rahisi kuliko wakati wote hata kama mpira unadunda kwa wachambuzi wa soka
zilikuwa ni kuhusiana na Bayern Munich kuitoa Manchester United kwa urahisi.
Mechi
ya kwanza ilipangwa kupigwa Old Trafford, ikaonekana ni kazi rahisi kwa Bayern
na kilichokosewa ni kitu kidogo tu. Wengi waliamini Wajerumani hao wangeshinda
hata wakiwa ugenini jijini Manchester, mechi ikaisha kwa sare ya bao 1-1.
Baada
ya hapo, kiasi fulani kukawa na mabadiliko ya hisia, kwamba inawezekana Man
United wakapindukia kabati na kuwavua ubingwa mabingwa hao, kitu ambacho
kilikuwa ni sawa na ndoto za alinacha.
Kwani
katika mchezo wa pili uliopigwa nchini Ujerumani, juzi usiku, United walikiona
cha moto kwa kulambwa mabao 3-1 na kuondolewa rasmi kwenye michuano hiyo
mikubwa Ulaya.
Ukiangalia
takwimu kwa maana ya mwenendo wa timu hizo, lilikuwa ni jambo la kubahatisha
kupita kiasi kuamini Man United ingewang’oa Bayern.
Kikosi
hicho cha David Moyes, kilisafiri kwenda Munich kikiwa na gumzo la tegemeo la
mchezaji mmoja tu, Wayne Rooney.
Lakini
kama ukizungumzia Bayern, utataja zaidi ya wachezaji sita ambao ni hatari na
wana uwezo wa kutengeneza matokeo kwa uwezo binafsi, angalia; Arjen Robben,
Frank Ribery, Thomas Muller, Mario Gotze, Mario Mandzukic, Thiago Alcantara na
wengine.
Sasa
piga hesabu kwa Man United ambayo ina sura ya mtu mmoja, isiyo na kiungo nyota
mchezeshaji au mkabaji. Wala winga hatari au mshambuliaji msaidizi kwa Rooney
hasa inapotokea Robin van Persie, yuko nje.
Man
United kushinda kwa Bayern, ilikuwa ni sawa na gari kubwa la mizigo aina ya
Fiat kutaka kulazimisha kuupanda Mlima Kitonga kwa kasi ya kilomita 60 kwa saa.
Inajulikana gari aina hiyo likipanda basi spidi 10 ndiyo saizi yake!
Ukizungumzia
kwa maana ya ukubwa wa majina ya timu, hazipishani kwa kuwa rekodi zake
zinaingia kwenye historia ndefu ya mafanikio. Lakini hali halisi na kipindi
husika, Bayern dhidi ya Man United ilikuwa ni vita ya Daudi na Goliath.
Lakini
kuna mambo mengine ya kiufundi yaliyokuwa yanaonyesha Man United kuvuka dhidi
ya Bayern ni kwa asilimia 15 tu. Angalia maboksi haya ya asilimia.
Bayern:
Msimu huu
katika ligi; Bayern Munich imeshinda 86% ya mechi zake, imeshinda 93% ya mechi
za nyumbani, imeshinda 80% ya mechi za ugenini.
Bayern
Munich imefunga mabao kwa 100% ikiwa nyumbani, imefunga mabao ugenini kwa 93%, Bayern
kwa 76% imekuwa ya kwanza kufunga mabao katika mechi zake na kwa 59% imeongoza
hadi mapumziko.
Bayern imefunga
bao katika kila mechi kati ya 14 zilizopita, isipokuwa moja ambayo ilikuwa ya
kwanza kwao kupoteza kabla ya kuivaa Man United.
Man Utd:
Msimu huu
katika ligi; Man Utd imefunga angalau bao moja kwa 88% katika mechi zake za nyumbani na imefunga bao
moja angalau kwa 61% kwa mechi zake za ugenini.
Man
United imeshinda mechi za 4 zilizopita za ugenini pia haijafungwa katika katika
ligi, Man Utd haijafungwa hata bao moja katika mechi zake 5 za ugenini ambayo
ni 100% ya kutopoteza nje, zilizopita za ugenini pia.
Bayern:
DATA ZA LIGI
MSIMAMO:
Tayari Mabingwa
MECHI 4 ZILIZOPITA:
FC Augsburg 1-0
Bayern
Bayern 3-3 Hoffenheim
Hertha Berlin 1-3
Bayern
FSV Mainz 0-2
Bayern
Man United:
DATA ZA LIGI:
MSIMAMO:
Nafasi ya 7
MECHI 4 ZILIZOPITA:
Newcastle 0-4 Man
Utd
Man Utd 4-1
Aston Villa
Man Utd 0-3 Man City
West Ham 0-2 Man
Utd
0 COMMENTS:
Post a Comment