Na Saleh Ally
MANCHESTER
United ndiyo ilikuwa timu inayosifika kwa kuwa na nafasi ya kupata mikwaju
mingi ya penalti katika kipindi cha ndani ya dakika 90.
Kikosi
hicho wakati kipo chini ya Alex Chapman Ferguson, kilikuwa kina sifa ya kuwa na
ubora, fowadi kali lakini walikuwa wakifanikiwa kupata penalti nyingi ndani ya
dakika 90.
Hali hiyo
ya kupata penalti nyingi ilikuwa ikifanya watu wengi kulaumu kuhusiana na Man
United kwamba imekuwa ikipata pointi nyingi kupitia mikwaju ya penalti.
Lakini sasa
mambo yanaonekana yamehamia Anfield kwa kuwa Liverpool ndiyo timu inayoongoza
kwa kupata mikwaju mingi ya penalti.
Kabla ya
mechi ya jana dhidi ya West Ham, Liverpool ilikuwa inaongoza kwa kupata mikwaju
nane ya penalti iliyokuwa imetumbukizwa wavuni.
Idadi hiyo
ni zaidi takribani asilimia 11 ya mabao yake 89 iliyoyafunga katika mechi zake
33 za ligi hiyo. Kwa kuwa katika mechi ya jana dhidi ya West Ham, Liverpool walipata penalti nyingine mbili.
Kasi ya
ufungaji ya washambuliaji wake wawili, Luis Suarez mwenye mabao 29 na Daniel
Sturridge mwenye 20, maarufu kama SAS iko juu sana.
Lakini
wadau wa soka wamemlaumu Suarez kwamba amekuwa anaongoza kujiangusha, kitu
ambacho ni sawa na ulaghai ambao unaiongezea Liverpool rundo la mikwaju ya
penalti.
Liverpool
imefunga penalti hizo kumi na kufungwa
mbili tu, hivyo kuwa timu iliyopewa mikwaju mingi zaidi na waamuzi wakati ligi
hiyo ikiwa inaenda ukingoni.
Man City
inafuatia baada ya kupata penalti sita, huku ikiwa imefungwa mkwaju mmoja tu wa
penalti. Chelsea inashika nafasi ya tatu kwa kuwa na mikwaju mitano wakati haijawahi
kufungwa hata mkwaju mmoja.
Manchester
United iliyokuwa kinara, sasa ina mikwaju minne tu iliyofunga huku ikiwa
imefungwa penalti mbili. Maana yake ni, ina nusu ya ile ya Liverpool.
Crystal
Palace, Sunderland na Tottehham Hotspur kila moja pia imepata mikwaju hiyo
minne kama ya Man United ambayo inaiondoa timu hiyo kwenye kundi la timu zinazopata
penalti nyingi sana kwa msimu.
Ila Palace
pamoja na kupata penalti nne, ina rekodi mbaya kwani imefungwa penalti sita
ukilinganisha na Spurs iliyofungwa tatu na Sunderland mbili.
Hata hivyo,
mshambuliaji nyota wa zamani wa Liverpool, Michael Owen, amesema mara nyingi
fowadi yenye washambuliaji wakali na wasumbufu ndiyo yenye nafasi ya kupata
penalti nyingi.
Wakati
akifanya uchambuzi wa Premiership kwenye runinga ya Sky Sports, Owen amesema kama
timu inashambulia sana na ina washambuliaji wenye kasi na uchu wa mabao,
uwezekano wa kupata rundo la penalti ni kawaida.
Fin.
0 COMMENTS:
Post a Comment