April 7, 2014





Kiungo nyota wa zamani wa Simba, Mwinyi Kazimoto, amezidi kuula baada ya kuongezewa mkataba na timu yake, Al Markhiya ya Qatar.


Kazimoto ameongezewa mkataba wa mwaka mmoja na klabu yake hiyo ambayo iko katika haraka za kupambana kupata nafasi ya kucheza Ligi Kuu nchini humo.

Akizungumza na SALEHJEMBE, Kazimoto amesema amefanikiwa kuongezewa mkataba na sasa utamazika mwaka 2015.

“Awali mkataba ulikuwa unamalizika mwezi wa sita mwaka huu, lakini tulikaa na kujadili suala hilo, sasa wamenipa mkataba mwingine wa mwaka mmoja,” alisema.

Kazimoto amekuwa tegemeo kubwa katika safu ya kiungo ya Al Markhiya ambayo msimu huu imeonekana kuwa na kikosi chenye ushindani.

Kocha wa Al Markhiya ameonyesha kumuamini Kazimoto na ndiye amekuwa akipewa kazi ya kuichezesha timu na pia kupata nafasi ya kuachia mashuti yake.

Kazimoto alinunuliwa na Al Markhiya akitokea Simba ambayo pia ilimsajili kutoka Ruvu Shooting iliyomuibua baada ya kujiunga nayo akitokea kwao Mwanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic