Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya umefanikiwa kuwa wa pili katika
viwanja vinavyotumiwa na timu za ligi kuu kwa kuweza kuingiza mapato mengi katika
mzunguko huu wa pili wa Ligi Kuu Bara.
Mpaka sasa, uwanja huo umeingiza kiasi cha Sh 195, 454, 000.00 ambazo
ni sawa na asilimia 15.98.
Sokoine, katika msimu huu kwa mara ya kwanza imekuwa ikitumiwa na
timu mbili ambazo ni wawakilishi wa mkoa huo, Tanzania Prisons na Mbeya City na
kwa mara ya kwanza imeingiza kiasi kikubwa namna hiyo, ikiwa ni baada ya Mbeya
City kupanda daraja.
Katika viwanja vyote, Uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam, ndiyo wa
kwanza na siku zote huwa unafanya vyema lakini Sokoine umeanza kuleta changamoto
kutokana na kufanya vizuri kwa timu ya Mbeya City.
Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wa Arusha ni wa mwisho, ukiwa
umeingiza Sh milioni 1,890,000.00 katika mzunguko wa pili, sawa na asilimia
0.15. Uwanja huo hutumiwa na JKT Oljoro pekee.
Uwanja wa Chamazi, unaotumiwa na vinara wa ligi, Azam pamoja na Ashanti
United na JKT Ruvu, wenyewe umeingiza Sh 17,166,000.00 ukishika nafasi ya sita.
0 COMMENTS:
Post a Comment