Mshambuliaji wa kimataifa wa Simba,
Mrundi, Amissi Tambwe, amewataka viongozi wa klabu hiyo kutafakari mara mia
maombi yake ya kumwongezea maslahi na kama wakipuuza, basi yeye ataondoka na
kwenda kujiunga na timu nyingine ambazo zinamhi.
Tambwe amesema anataka mshahara kama
anaolipwa kiungo mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Okwi.
Okwi analipwa na Yanga kwa mwezi dola 4,000,
zaidi ya Sh milioni 6, wakati Tambwe analipwa na Simba dola 1,000, zaidi ya Sh
milioni 1.6.
Hali hiyo imekuwa ikimuumiza kichwa mchezaji
huyo na kuutaka uongozi wa Simba kumwongezea maslahi kama anayopewa Okwi na
Yanga kwa sababu kiwango chake ni
bora zaidi ya mshambuliaji huyo raia wa
Uganda.
Tambwe amesema kuwa yeye amekuja Tanzania kutafuta fedha, hakuja kuuza sura,
hivyo ameutaka uongozi wa Simba kumwongezea maslahi ili aweze kuendelea
kuitumikia klabu hiyo iliyomsajili akitokea Vital’O ya Burundi.
Alisema endapo uongozi huo utapuuza
maombi yake hayo, basi ataondoka na kwenda kujiunga na timu nyingine ambazo
alidai kuwa anaendelea kufanya nazo mazungumzo kupitia kwa wakala wake ambaye
sasa yupo jijini Dar es Salaam.
“Simba naipenda sana lakini wasipotaka
kusikiliza maombi yangu niliyowaambia basi mimi nitaondoka na sisemi haya kwa
kutania.
“Nimekuja Tanzania kutafuta pesa, sikuja
kuuza sura, nachotaka ni maslahi mazuri ili niendelee kuitumikia Simba, kama
wasipofanya hivyo nitaondoka zangu na wala siogopi kwani timu hiyo siyo ya baba
yangu,” alisema Tambwe ambaye anaongoza kwa kuzifumania nyavu, akiwa na mabao
19.
Hata hivyo, uongozi wa Simba kupitia kwa
katibu wake mkuu, Ezekiel Kamwaga umemtaka Tambwe kutulia na kufanya kazi yake.
“Tambwe anatakiwa kutulia na kufanya kazi
yake, kwani tumeshajua ni jambo gani ambalo anahitaji, taratibu zipo hivyo
inabidi azifuate na siyo kuongea katika vyombo vya habari,” alisema Kamwaga.
0 COMMENTS:
Post a Comment