MASHABIKI WA YANGA NA SIMBA |
Zile kelele za kila mmoja ni mbabe
kuliko mwenzake zimemalizika kwa sare ya bao 1-1.
Yanga na Simba, hakuna mbabe na hakuna
anayeweza kumtambia mwenzake tena baada ya sare hiyo ya kufunga Ligi Kuu Bara
kwenye Uwanja wa Taifa, leo.
Mabao yote yamepatikana katika kipindi
cha pili tena dakika 10 za mwisho baada ya Simba kufunga lao katika dakika ya
82 kupitia Haruna Chanongo.
Lakini Yanga, wakasawazisha dakika ya 85
kupitia kwa Simon Msuva aliyepokea pasi ya Didier Kavumbagu.
Mechi hiyo ilikuwa na vivutio vingi na
Simba walionekana kuutawala mpira katika kipindi cha kwanza.
0 COMMENTS:
Post a Comment