Mshambuliaji wa Simba, Betram Mwombeki,
ameifungia vioo klabu yake ya Simba na kuamua kufanya mambo yake kwa sasa
kutokana na kutokuwa na nafasi katika
kikosi cha kocha mkuu wa timu hiyo, Mcroatia, Zdravko Logarusic.
Mwombeki ambaye alipata kutamba sana
mwanzoni mwa msimu huu wakati timu hiyo ikiwa chini ya kocha Abdallah Kibadeni,
amekuwa na wakati mgumu tangu kikosi hicho kiwe chini ya Logarusic.
Mwombeki amesema kwa sasa yupo nyumbani anafanya shughuli zake kwa ajili ya
maisha yake ya baadaye.
Alisema kuhusiana na sababu za
kutoonekana katika kikosi cha timu hiyo, hawezi kuzizungumza kwa sasa lakini
atafanya hivyo muda utakapofika, ikiwa ni pamoja na hatma yake ndani ya klabu
hiyo.
“Haya ni mambo yangu binafsi, hivyo siwezi
kuyazungumza kwa sasa lakini muda ukifika nitazungumza na kila mtu atajua nini
hatma yangu katika kikosi cha Simba.
“Hivi sasa sionekani Simba kutokana na
sababu mbalimbali lakini kubwa zaidi ni kwamba nilikuwa naumwa ila sasa
naendelea vizuri, pia kuna baadhi ya mambo yangu binafsi ninafanya,” alisema
Mwombeki.
0 COMMENTS:
Post a Comment