Pamoja na kulipwa mamilioni ya fedha na klabu yake ya Arsenal,
mshambuliaji Lukas Podolski ameonyesha hana makuu na anapenda maisha simpo.
Mjerumani huyo nyota pia wa timu yake ya taifa, ameonekana
akikwea daladala za mji wa London kama kawa.
Jana asubuhi, Podolski alipanda basi No 26 linalokwenda kutoka Hackney
Wick likikatiza maeneo mbalimbali ya jiji la London hadi stesheni ya Waterloo.
Si kawaida kwa wachezaji nyota na hasa wa timu zinazoshiriki Ligi
Kuu England kupanda mabasi.
Katika moja ya picha, utaona Mjerumani huyo akizozana na shabiki
aliyetaka wapige picha wakati yeye alionyesha ana haraka.
0 COMMENTS:
Post a Comment