Baada ya
Rhino Rangers na JKT Oljoro kupunga mkono wa kwa heri Ligi Kuu Bara, sasa
imebakia nafasi moja kati ya Tanzania Prisons ya Mbeya, Ashanti ya Dar au
Mgambo ya Tanga, yoyote inaweza kushuka daraja.
Prisons na
Ashanti zinatarajia kukipiga kesho Jumamosi kwenye mechi ya mwisho ya Ligi Kuu
Bara kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ambapo timu zote zina pointi 25, lakini
sare au kufungwa kwa Ashanti kutamaanisha kuwa timu hiyo nayo rasmi imeshuka
daraja.
Prisons
inahitaji sare yoyote au ushindi ili ibaki ligi kuu, wakati Ashanti inahitaji
ushindi wowote ili ijihakikishie kubaki, Mgambo ambayo inacheza dhidi ya Mbeya
City ikifungwa kwa tofauti ya mabao mawili huku Ashanti na Prisons zikipata
sare, maana yake ni kuwa Mgambo itashuka kwa kuzingatia tofauti ya mabao ya
kufunga na kufungwa.
Nahodha wa
Ashanti, Abuu Mtiro amesema wamepata nguvu baada ya kuifunga Simba na wanaenda
kupambana na Prisons kwa nguvu zote. “Mchezo wa Jumamosi utakuwa mgumu kwa
sababu wote tuna pointi sawa, hivyo tunahitaji ushindi ili tuweze kubaki ligi
kuu.
“Ushindi
tulioupata dhidi ya Simba ndiyo umetupa matumaini kupata nafasi ya kubaki na
tutajitahidi kuhakikisha msimu ujao tunashiriki tena ligi kuu,” alisema
Mtiro.
Msimamo ulivyo
P GD
Pts
10. Mgambo 25 -16 26
11. Prisons 25 -8 25
12. Ashanti 25 -18 25
13. Oljoro 25 -18 18
14. Rhino 25 -19 16
0 COMMENTS:
Post a Comment