Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea kesho (Aprili 9 mwaka huu) huku
timu za Azam na Yanga ambazo zipo nafasi mbili za juu zikiendelea kuchuana.
Kila timu
na hasa Yanga na Azam zinahitaji pointi tatu za kesho kwa udi na uvumba.
Yanga
inajaribu kuhakikisha haifanyi makosa kama katika mechi dhidi ya Mgambo ambayo
ililala kwa mabao 2-1 mjini Tanga.
Lakini Azam
FC itakuwa vitani kuhakikisha inapata pointi sita ili ichukue ubingwa kwa mara
ya kwanza, hivyo ni lazima izibebe pointi tatu za kesho ili kubakiza tatu tu.
Azam itakuwa mgeni wa Ruvu Shooting
katika mechi itakayochezwa kwenye Uwanja wa Mabatini uliopo Mlandizi mkoani
Pwani. Nayo Yanga itakuwa mwenyeji wa Kagera Sugar katika Uwanja wa Taifa
jijini.
Yanga, Azam, Ruvu Shooting na Kagera
Sugar zote zimeshinda mechi zao za raundi ya 23 wakati mechi za kesho zitakuwa
kwa ajili ya kukamilisha raundi ya 24 ya ligi hiyo ambayo inatarajia kukamilika
Aprili 19 mwaka huu.
Ligi hiyo itaingia raundi ya 25
Aprili 12 na 13 mwaka huu ambapo timu zote 14 zitakuwa viwanjani. Aprili 12
mwaka huu itakuwa Mtibwa Sugar vs Ruvu Shooting (Manungu, Morogoro), Coastal
Union vs JKT Ruvu (Mkwakwani, Tanga), na Tanzania Prisons vs Rhino Rangers
(Sokoine, Mbeya).
Aprili 13 mwaka huu ni Mgambo
Shooting vs Kagera Sugar (Mkwakwani, Tanga), Simba vs Ashanti United (Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam), Mbeya City vs Azam (Sokoine, Mbeya) na Oljoro vs Yanga
(Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha).
0 COMMENTS:
Post a Comment