April 8, 2014

Mtindo wa ushangiliaji wa mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Emmanuel Adebayor umechukua umaarufu mkubwa katika mitaa ya jiji la London.

Adebayor raia wa Togo amekuwa akishangilia kwa mtindo wa kupiga saluti.
Kutokana na kuendelea kufanya vizuri katika kikosi cha Spurs, mashabiki wengi wa timu hiyo na wengine wa jiji la London wamekuwa wakivutiwa sana.
Hivyo, wengi wao wakitajiwa jina la Adebayor, basi huinua mikono yao na kupiga saluti.
Tayari wachezaji wenzake wa Spurs wamekuwa wakimpigia saluti na hata benchi la ufundi na Kocha wa Spurs, Tim Sherwood naye anaikubali saluti hiyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic