April 19, 2014


Kipa namba moja wa Yanga, Deogratius Munishi ‘Dida’, ameeleza kuwa katika mchezo wa leo dhidi ya Simba, atahakikisha mshambuliaji Amissi Tambwe hapati bao.


Dida anatarajiwa kukaa langoni leo katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara msimu huu dhidi ya watani wao wa jadi Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Dida amesema atawapanga vizuri mabeki wake kuhakikisha Tambwe hafungi bao lolote hata la kuotea.


“Ninajua mchezo utakuwa mgumu lakini nina imani mabeki wangu watanilinda vizuri na kuhakikisha wanazuia kikamilifu mashambulizi ya Simba na kutotoa nafasi kwa Tambwe kufunga bao lolote.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic