Azam TV yawakumbuka mashabiki wa soka
nchini
Runinga ya Azam TV leo imezundua shindano la kumtafuta shabiki namba
moja wa soka hapa nchini ambaye atajinyakulia kitita cha Sh. 10 milioni.
Mchakato huo wa kumpata shabiki huyo
unatarajia kuanza Jumamosi hii katika viwanja vya Leaders, jijini Dar es Salaam
ambapo mashabiki wote wa soka hapa nchini wanatakiwa kufika kwa lengo la
kufanyiwa usaili.
BOSI WA AZAM TV, TORRINGTON |
Mratibu wa shindano hilo, Wasiwasi Mwabulambo ameimba SALEHJEMBE kuwa mashabiki 10 watakaofanya vizuri katika usaili huo watakautanishwa ndani ya nyumba moja kwa siku 30 na mmoja kati yao ataibuka mshindi wa shindano hilo ambalo limepewa jina la Kwetu House (Seach for the ultimate fan).
“Usaili kwa ajili ya shindano hilo
utaanza 3.00 asubuhi mpaka saa 11.00 jioni, watu wanapaswa kushiriki ni wanaume
pekee wenye umri kuanzia miaka 18, wanawake na watoto haruhusiwi.
“Mbali na hayo, pia kwa mwaka huu
shindano hilo litashirikisha mashabiki wa Dar es Salaam kwa sababu ndiyo kwanza
tuanza lakini mwakani tutalipanua zaidi liwe la nchi nzima,” amesema
Mwabulambo.
Mashabiki hao wataishi kwenye nyumba
mfano wa wale ambao hushiriki katika shindano la Big Brother.
Mshindi wake ataibuka na kitita cha
Sh milioni 10 taslimu na mwakani litaendelea kwa kushirikisha mikoa mingine.
Wakati likiendelea, watu wataendelea
kulishuhudia kupitia ving’amuzi vya Azam TV.
0 COMMENTS:
Post a Comment