Timu ya Tanzania ya
umri chini ya miaka 15 imewasili salama jijini Gaborone, Botswana kwa ajili ya
michezo ya Afrika ambapo itacheza mechi yake ya kwanza Mei 22 mwaka huu dhidi
ya Mali.
Kikosi hicho cha
wachezaji 16 chini ya Kocha Abel Mtweve kimetua jijini Gaborone jana (Mei 19
mwaka huu) jioni kwa ndege ya South African Airways. Michezo hiyo itamalizika
Mei 30 mwaka huu.
Wachezaji waliopo
kwenye kikosi cha Tanzania ni Adam Shayo, Amani Ally, Amos Manguli, Amri Nyuki,
Amede Amani, Baraka Rashid, David Uromi, Goodlove Mdumule, Hance Msonga, Kelvin
Kamalamo, Makalius Amrin, Nasson Chanuka, Paulo Ngowi, Petro Shaban, Rajab
Mohamed na Thomas Chindeka.
Nchi nyingine
zinazoshiriki michezo hiyo kwa upande wa mpira wa miguu ni Afrika Kusini,
Botswana, Nigeria, Mali na Swaziland.
Gabon na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC)
ambazo nazo zilikuwa zishiriki kwenye michezo hiyo katika dakika za mwisho.
0 COMMENTS:
Post a Comment