May 30, 2014



KINGEKUWA ni kitu cha kishabiki, basi ningeweza kusema mambo sasa yananoga ile mbaya kwa kuwa unakoelekea uchaguzi mkuu wa Simba, haina ubishi ni dalili mbaya.


Simba inahitaji maendeleo zaidi ya malumbano, lakini dira ya uchaguzi mkuu wa viongozi uliopangwa kufanyika Juni 29 unaonyesha kuwa klabu hiyo imegawanyika kwa makundi.
Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali alisema kuna makundi saba, lakini kwa sasa kuna makundi mawili ambayo yanaonekana yamejitenga na kila upande kuna wapambe.
Tena kuna wapambe ambao hata kura hawatapiga kwa kuwa si wanachama au ni wanachama lakini si hai, lakini wamekuwa wakiandamana na viongozi hao na wengine wakiwa wamebeba mabango kuwapinga wengine au kusema maneno ya kashfa dhidi yaw engine.
Upinzani uliopo kuelekea uchaguzi mkuu wa Simba si wa kisayansi, lakini unaonyesha umejaa uadui, watu wanataka kuonyeshana mbavu zao na wengine uwezo wa elimu zao.
Upinzani mkubwa uko katika makundi mawili, moja linaongozwa na Evans Aveva, jingine linaongozwa na Michael Wambura na hawa kila mmoja anaonekana kuwa ana nafasi ya kushinda ingawa asilimia za ushindi zinaweza kuwa na utofauti kutokana na hali halisi.
Hatujui atashinda yupi, lakini uchaguzi hauna mwenyewe. Lakini tayari Simba wameonyesha kuwa hawataungana tena kwa kuwa mwenendo wa kampeni unavyokwenda, umejaa uadui, hali ya kutopendana na ubabe ambao hauna sababu.
Ninaamini iwapo atashinda Aveva ambaye kweli ana uzoefu na amekuwa katika Simba ambayo imefanya vizuri kipindi akiwa kiongozi kwenye kamati ya usajili, lakini bado atahitaji mchango wa Wambura ambaye pia ameongoza sehemu kadhaa.
Mfano Aveva akiwa rais, huenda mawazo ya Wambura yanaweza kusaidia hata kidogo. Halikadhalika kwa Wambura akishinda, lakini kwa hali ilivyo sasa, hakuna atakayesaidia.
Kwa kuwa Aveva amekuwa kimya sana, unaweza usimuingize kwenye kundi hilo lakini bado haitoshi kuacha kuamini kwa tayari Simba imegawanyika na tayari hakuna upendo.
Nani anaweza kusema sehemu isiyokuwa na upendo inaweza kupata mafanikio? Si lahisi kwa kuwa watu wako kwa makundi na hawashirikiani kwa ukaribu. Hii ni dalili kuwa maisha ya Simba kwa miaka mingine minne ijayo yatakuwa na ugumu.
Uchaguzi ni kitu cha kidemokrasia, lazima kwa wagombe na wale wapambe wakubali kufuata utaratibu na hasa kanuni na sheria kwa mujibu wa katiba yao.
Lakini maneno ya kashfa, maneno ya vitisho na hata kutaka kudhalilishana haiwezi kuwa njia sahihi ya ujenzi. Baada ya uchaguzi, lazima Simba irudi kuwa moja ili mambo yaende vizuri.
Kuna kashfa zimeanza kutolewa za elimu, lakini ukiangalia kwa viongozi waliopita wa Simba hasa wale waliopata mafanikio ya juu wakiwa na klabu hiyo tokea miaka ya 1930, hawakuwa na elimu ya juu.
Bado viongozi hao na elimu yao iliyoonekana ni ya chini. Waliisaidia Simba hadi kujenga majengo hata kama ni kwa vipindi tofauti. Hata Ulaya si watu wote ni wanaolingana na elimu na wenye elimu ya juu pekee ndiyo wenye mafanikio, hivyo kashfa na kukatishana tamaa hakutakuwa sahihi.
Uchaguzi unaweza kufanyika kwa utaratibu na mipango ya uhakika, kukawa na staha na mwisho atakayeshindwa akawa tayari kuingia na kumsaidia aliyeshinda kwa ajili ya mafanikio ya klabu hiyo kwa kuwa anayeshindwa, bado anabaki kuwa mwanachama wa Simba, hapaswi kujitenga, akifanya hivyo utakuwa ni uroho wa madaraka.
FIN.
Loga asajili watano wa timu za taifa
Na Martha Mboma
KOCHA Zdravko Logarusic amesema anataka Simba kusajili wachezaji watano wa kimataifa ambao watakuwa wanacheza katika timu za taifa na si vinginevyo.
Akizungumza kutokea katika mji ulio kilomita 400 kutoka jiji la Zagreb, Loga ameiambia Championi Ijumaa, wachezaji watano wa kulipwa wa Simba, kila mmoja anapaswa kuwa katika kikosi cha timu yake ya taifa.
“Lengo la Simba ni kufanya vizuri na kama utasajili wachezaji kutoka nje, lazima kila mmoja awe kwenye kikosi cha timu yake ya taifa.
“Sitaki mchezaji ambaye atakuja Simba halafu akae kwenye benchi, nimeamua kufanya hivi ili kuwa na wachezaji wa kimataifa ambao ni msaada,” alisema.
Logarusic ambaye yuko mapumzikoni nyumbani kwao Croatia, amesisitiza kwamba  kama Simba itasajili wachezaji kutoka Tanzania, lazima wawe majembe.
Hata hivyo, taarifa nyingine zinameeleza katika ripoti yake ya nusu msimu uliopita, alisisitiza wachezaji watatu wa kimataifa wabaki.
Aliwataja anaotaka wabaki kuwa ni Donald Musoti, Joseph Owino na Amissi Tambwe ambaye ameibuka kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara.
Hivyo, Loga atakuwa na kazi ya kusaka wachezaji wawili tu kutoka nje ya Tanzania ili kutimiza idadi ya watano kwa mujibu wa kanuni za TFF.
Hata hivyo, uhakika wa kocha huyo kurejea Simba ni baada ya uchaguzi na tayari Zacharia Hanspope ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya usajili alimpa dola 8,000 ili aweze kuamini kwamba klabu hiyo inamhitaji kweli.



1 COMMENTS:

  1. UCHAGUZI WA SIMBA MLISHAUHARIBU NYIE WAANDISHI BAADHI YENU KWA KUMPENDA KD KUPITA KIASI NA KUAMINI BILA KD AU KIBARAKA WAKE YEYOTE SIMBA HAIENDI,NA HIYO HALI YA KUWAFANYA MUAMINI HIVYO IMEWEKWA PURPOSELY NA KD NA GENGE LAKE KWA KUHUJUMU UONGOZI WOWOTE SIMBA AMBAO HAUTOKANI NA WAO,TUMEONA WALIVYOUANDAMA UONGOZI WA ADEN MPAKA WAKAHAKIKISHA ADEN NA KABURU WANAVURAGANA NA HAIKUTOSHA KUTWA IKAWA NI KUMCHAFUA ADEN KWA KUWATUMIA NYIE HASA WEWE,HUO NDIO UKWELI SALEH HATA UKICHUKIA POA BUT LAZIMA WATU WACHACHE WA KUSEMA UKWELI TUWEPO,NA NINAKWAMBIA CHUKUA MANENO YANGU KABURU NA KD(AVEVA) HAWAWEZI KUFANYA KAZI PAMOJA,I KNOW THEM,NAUJUA MSIMAMO WA KABURU NA HASSANOO KUHUSU KD NA GENGE LAKE(AVEVA,MLAMU NA WENGINE WA FOS,KUNA FOS NDANI FOS SI WAMOJA AS YOU GUYS THINK

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic