Klabu ya TP Mazembe
imewaruhusu wachezaji wake Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu kujiunga na timu
ya Taifa (Taifa Stars) ambayo tayari imewasili Harare, Zimbabwe kwa ajili ya
mechi ya michuano ya Afrika.
ULIMWENGU AKIPAMBANA |
Taifa Stars itacheza na
Zimbabwe (Mighty Warriors) katika mechi ya marudiano raundi ya mchujo kuwania
tiketi ya kucheza Fainali za Afrika zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Mechi hiyo itachezwa Jumapili (Juni 1 mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Harare.
Samatta na Ulimwengu watawasili Harare kesho (Mei
30 mwaka huu) saa 3.40 usiku kwa ndege ya Kenya Airways.
Watajiunga na TP
Mazembe mara baada ya mchezo huo ambapo Juni 2 mwaka huu watakwenda moja kwa
moja Ndola, Zambia ambapo timu yao imepiga kambi kwa ajili ya mechi za Ligi ya
Mabingwa Afrika.
0 COMMENTS:
Post a Comment