Kocha wa zamani wa Yanga, Hans van der Pluijm amesema bado
anawasubiri Yanga baada ya kufanya mazungumzo na wachezaji.
Akizungumza na SALEHJEMBE kutoka Accra, Ghana, Pluijm alisema amefanya
mawasiliano na wachezaji kadhaa kwa ajili ya kujiunga na Yanga.
Hivyo suala la wajiunge nayo au la, litabaki kwa Yanga
wenyewe.
“Nitakuwa hapa Accra kwa wiki kadhaa kabla ya kwenda Saudi
Arabia. Sasa inategemea wao Yanga wanatakanini.
“Kwa kifupi kazi yangu nilimaliza na uamuzi wa mwisho ni
wao,” alisema Pluijm.
Alipoulizwa suala kuhusiana na mshahara wake anaowadai
Yanga, alisema: “Nafikiri tuliache kwanza, Yanga wana mpango wa kulimaliza
vizuri.”
0 COMMENTS:
Post a Comment