Mgombea wa nafasi ya makamu wa urais katika
klabu ya Simba amesema anaidai klabu hiyo zaidi ya Sh milioni 200.
Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema anadai
kitita hicho kilichotokana na kuvunja mkataba wakati akiwa kocha, lakini madai
ya mishahara na marupurupu yake.
“Tokea enzi za uongozi wa (Hassan) Dalali,
Simba ina fedha zangu na hadi leo hawajanilipa.
“Zaidi ya Sh milioni mia mbili, nawadai na
hata mzee Dalali analijua hilo, hivyo ninataka kulipwa.
“Wasipofanya hivyo sitakuwa na msamaha,
nitawapeleka mahakamani,” alisema Julio.
Julio amechukua fomu za ugombea nafasi ya
makamu na kufanikiwa kurejesha kwa wakati mwafaka.
Sasa atapambana na Swedi Nkwabi pamoja na
Geofrey Nyange ‘Kaburu’.
Kwa maana hiyo anataka azirudishe hela zake anazozidai simba kwa kupitia uongozi endapo atachaguliwa? Kwa sababu ikiwa anaidai simba kwa nini angojee wakat wa uchaguzi tena kipind cha kuchukua fomu ya kugombea uchaguzi ndo akumbushie deni? Huyu c kiongozi ni mchumia tumbo lake na akipata uongozi basi atazirudisha fedha zake kwa njia anayoijua yeye
ReplyDelete