Imefahamika kuwa
uongozi wa Yanga ulipanga kumpotezea aliyekuwa mshambuliaji wake, Didier
Kavumbagu ambaye hivi karibuni alitua Azam FC kwa mkataba wa mwaka mmoja.
Habari za uhakika
kutoka ndani ya Yanga zimedai kuwa, uongozi huo wa Yanga ulikuwa ukimfanyia
hivyo Kavumbagu ambaye ni raia wa Burundi kwa sababu ulikuwa umeshamuondoa muda
mrefu katika mipango yake kwa ajili ya msimu ujao kwa madai ya kutoridhishwa na
aina ya uchezaji wake.
“Hali hiyo ndiyo
iliufanya uongozi kukaa kimya bila ya kuchukua jitahada zozote za kumwongezea
mkata tofauti na ilivyokuwa kwa nyota wengi wa kimataifa wa klabu hiyo, Hamis
Kiiza na Haruna Nyionzima.
“Hata hivyo jamaa ana
bahati sana kama asingekuwa makini na kuchukua maamuzi hayo ya kujiunga na Azam
mapema akaendelea kuisubiri Yanga, angeumbuka kwani hakukuwa na mpango wowote
wa kumbakisha,” kilisema chanzo.
Kuhusiana na hilo, Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu ambapo alisema:
“Hatukutaka
kumtelekeza Kavumbagu ila mpango wetu ulikuwa ni kwamba kama TFF ingeendelea
kusimamia mpango wake wa wachezaji watatu basi yeye pamoja na Mbuyu Twite
tungemwacha na kubakia na Kiiza (Hamis) pamoja na Niyonzima (Haruna).
“Kuondoka kwake na
kwenda kujiunga Azam, kwetu sisi tumechukulia kama jambo la kawaida na wala
halitumizi kichwa kwani ni mchezaji wa kawaida,” alisema Njovu.
Aidha, Njovu aliongeza
kuwa kwa sasa wapo katika mchakato wa kumtafuta straika ambaye atakuwa hatari
mara mbili zaidi ya Kavumbagu.
0 COMMENTS:
Post a Comment