Sare ya mabao 3-3 dhidi ya Crystal
Palace imetia gundu mbio za Liverpool kutwaa ubingwa we Ligi Kuu England tena mwishoni
kabisa.
Mashabiki wake walionekana kutoamini
baada ya timu yao kuongoza kwa mabao 3-0 dakika 11 kabla ya mpira kwisha mabao
yakaanza kurudi kama mvua hadi kufikia 3-3.
Vilio vikatawala, hawakuamini
kilichokuwa kinaendelea lakini hakuna ubishi ndiyo mpira, ndiyo maana unapendwa
lakini umekuwa ukiumiza watu na ndiyo ulivyo. Lakini machozi yao yameonyesha
mapenzi ya dhati.
0 COMMENTS:
Post a Comment